Barakah The Prince awakata ngebe mashabiki wa Alikiba

Kwa muda mrefu sasa wadau wengi wa muziki wa Bongo Fleva wamekuwa wakiamini kuwa Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince na mfalme wa Bongo Fleva, Alikiba wana bifu au tofauti miongoni mwao baada ya Baraka The Prince kujitoa kwenye lebo ya RockStar4000 ambayo ipo chini ya Alikiba na Meneja wake Seven Mosha.

Ukweli ni kwamba Barakah The Prince hana tofauti/bifu  yoyote na Alikiba kama ambavyo mashabiki wengi wa Alikiba na wadau wa muziki walivyokuwa wakidhania kwani  Hitmaker huyo wa Sometimes kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha hilo kwa kumtakia Kheri ya siku yake ya kuzaliwa Alikiba .
Happy Birthday kaka King Kiba nakutakia maisha marefu“ameandika Barakah The Prince kwenye posti ambayo imeleta majibu kwa baadhi ya wadau waliokuwa wakidhani kuwa msanii huyo ana bifu na Alikiba.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment