Dkt. Louis Shika atangaza neema kwa wanafunzi watakaofanya vizuri darasani

Bilionea Dkt. Louis Shika ambaye amejizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania baada ya kuibuka katika mnada wa kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi ametua leo alhamisi Novemba 23, 2017 mjini Kahama kwenda kuhudhuria katika mahafali katika chuo cha Afya cha (Kahama College of Health Science).

Dkt. Louis Shika akiwa katika matukio ya upigaji picha na wahitimu chuoni hapo.
Dkt. Shika akitoa hotuba kwenye sherehe za mahafali mbele ya wahitimu amesema anatambua kuwa masomo ya sayansi hususani ya Afya karo yake ni ghali hivyo ameahidi kuwalipia karo wanafunzi wote watakaofanya vizuri kwenye masomo yao chuoni hapo.
Natambua umuhimu wa masomo ya afya na ughali wa malipo yake kwa Watanzania wenye kipato cha chini, nitawalipia wanafunzi wote wenye uwezo darasani ambao wazazi au walezi wao hawana uwezo wa kugharamia masomo yao.“amesema Dkt. Shika wakati akitoa hotuba yake kwenye mahafali chuoni hapo.
Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Chuo hicho, Yona Bakungile ameeleza sababu za kumualika Dkt. Shika katika Chuo chake kuwa ni kutokana na utaalamu wake wa masuala ya tiba ya binadamu na umaarufu wake unaoendelea kuvuma nchini.
Chuo changu kinatoa mafunzo ya afya ya binadamu; licha ya umaarufu wake nchini kwa sasa, Dk Shika ni miongoni mwa wataalamu katika fani ya utabibu ndiyo maana nimemwalika. Naamini atawashauri na kuwapa hamasa wahitimu na wanafunzi wanaoendelea,” amesema Bakungile kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwananchi.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment