Hamisa Mobetto aibuka mshindi tuzo za Starqt

Mwanamitindo kutoka Tanzania,  Hamisa Mobetto amefanikiwa kunyakuwa tuzo ya Starqt Awards katika msimu wake wa nne kupitia kipengele  cha ‘People Choice Awards’.

Mrembo huyo aliyekuwa ana wakilisha Tanzania na Afrika Mashariki alikuwa akiwania vingengere viwili ambavyo ni ‘People Choice Awards’ na ‘Super Mum’ ila amefanikiwa kuibuka kidedea katika kipengele kimoja tu.


Starqt Awards ni tuzo zinazohusisha biashara, mitindo, burudani na vitu vingine. Na zoezi la ugawaji tuzo hizo lilifanyika Novemba 4 mwaka huu katika ukumbi wa Bedford View City Hall, mjini Johannesburg nchini South Afrika.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment