Hatimaye Zimbabwe yapata Rais mpya baada ya miaka 37 ya utawala wa Mugabe

Maelfu ya Raia nchini Zimbabwe leo wameshuhudia tukio la kihistoria la kuapishwa kwa Rais mpya wa taifa hilo, Emmerson Mnangagwa baada ya kukaa kwa miaka 37 chini ya utawala wa kiimla wa Robert Mugabe.

Emmerson Mnangagwa
Bw. Emmerson Mnangagwa ameapishwa kama rais wa Zimbabwe, kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Mzee Robert Mugabe .
Mnangagwa kwenye utawala wa Mugabe alihudumu nafasi ya makamu wa Rais na mapema mwezi septemba mwaka huu kufutwa kazi na Mugabe.
Kufutwa kwake kazi kulipelekea chama tawala cha Zanu-PF na jeshi kuingilia kati na kumlazimisha Mugabe ang’atuke madarakani.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment