Hii Kalii :: Harusi yavurugika baada ya mchepuko wa bwana harusi kujitokeza kanisani


Harusi ya mwanaume mmoja jijini Blantyre, nchini Malawi imeingia doa siku ya jumamosi ya wikiendi iliyopita baada ya mwanamke mmoja kusimama mbele ya kanisa na kudai kuwa bwana harusi ni mchumba wake na alimuahidi kumuoa.

Wanandoa wakiwa kwenye tukio la Harusi baada ya kurejea kutoka kanisani.
Kwa mujubu wa maelezo kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa limetokea katika kanisa la  Living Waters Church (LWC), Dayosisi ya Chilimba mjini Blantyre. Ambapo waumini wamesema walishtuka ghafla kumuona mwanamke huyo aliyekuwa amevalia suti akikimbia mbele ya altare baada ya Mchungaji kutangaza kuwa kama kuna mtu anapingamizi ajitokeze kanisani hapo.
Bi Harusi akitolewa na ndugu zake kanisani huku akiwa amevurugwa na tukio hilo.

Tukio hilo lilianza kusambaa kwenye mtandao wa Twitter  baada ya mdau mmoja kurusha picha hizo mtandaoni kabla ya kunaswa na vyombo vya habari.
Hata hivyo baada ya tukio hilo kutokea Mchungaji alilazimika kusimamisha zoezi hilo kwa muda lakini baadae Bi. Harusi alirejea na shughuli kuendelea. Ingawaje haijatolewa taarifa rasmi kuhusu mahusiano kati  ya Bwana Harusi mwanamke huyo aliyejitokeza kanisani hapo.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.