Madee akerwa na wanaodai ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya ni kiki

Msanii Madee ameonyesha kukerwa na baadhi ya watu hata wasanii ambao wanadai ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya ni kiki.

Madee ambaye ni kama Baba Mleze wa Dogo Janja ameiambia FNL ya EATV kuwa kitu hicho ni kibaya sana kwani kuna uwezekano msanii akawa anahitaji msaada wa haraka na watu wakachukulia hilo kama kiki.
“Kitu ambacho nimekigundua na ni kibaya na kinaendelea kutokea ni watu kuamini katika kiki, hata leo ikitokea nimegongwa na gari nakuumia watu bado wataamini ni kiki na kushindwa kunisaidia,” amesema Madee.
“So kama hili suala lingekuwa la kumsaidia Janja ili aokoke kwenye jambo labda ni baya basi tungekuwa tumeshamuumiza kwa sababu watu wote wanaamini kwenye kiki, hadi sasa watu wengi hawaamini kama Dogo Janja, hivi vitu vingine vya kusema kiki tuviache” ameongeza Madee.
Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa yao October, 28 mwaka huu kwa mujibu taarifa za mitandao ya kijamii lakini September 4 ndipo Dogo Janja aliweka wazi hilo kuwa wamefunga ndoa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment