Mnada wa Lugumi na masharti mapya kuwadhibiti akina ‘900 itapendeza'

Kampuni ya Udalali ya Yono imetangaza kuwa kesho, Novemba 24, 2017 itarudia upya mnada wa nyumba mbili za kifahari za mfanyabiashara Said Lugumi zilizoshindikana kuuzwa baada ya Dr. Louis Shika kuzinunua na kushindwa kuzilipia.

DK Shika akiwa kwenye mnada uliopita
Nyumba zilizotajwa kurudiwa kuuzwa katika mnada ni Plot. No 47, iliyopo Mbweni JKT,  na nyingine iliyopo Upanga.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart, Scholastica Kevela ameeeleza kuwa kwa sasa kampuni ya Yono imeweka masharti magumu ili kuhakikisha kwamba hakuna atakayeibuka kuuharibu mnada huo.
“Mchezo ule ambao tulichezewa mara ya mwisho hautarudiwa, kwa sasa tumekuja na masharti magumu kwamba, washiriki wote watakaoingia katika minada uwe mshangiliaji au mtazamaji lazima utajiandikisha katika kitabu maalumu cha washiriki wa mnada,” amesema Kevela.
Aliongeza “Baada ya kujiandikisha, tutakujazia fomu maalumu ya kushiriki mnada, tutakuchua taarifa mbalimbali kutoka katika vitambulisho vyako vya Taifa, leseni ya udereva au pasi ya kusafiria.”
“Kama kweli wewe ni mshiriki halali tutakutaka utoe Sh2 milioni kupitia akaunti ya Yono kama dhamana ya ushiriki kuwa unataka kununua nyumba, ukishinda mnada hiyo Sh2 milioni ni sehemu ya malipo na kama ukishindwa kupata mali au bidhaa tunakurudishia mara moja,” amesema.
Amesema kwa atakayeshindwa kupata mali na Sh2 milioni ametoa na kisha akaharibu mnada, hatarudishiwa fedha na hatua za kisheria zitachukuliwa. Amesema mshindi wa mnada atatakiwa kulipa papo hapo malipo ya awali ya asilimia 25.
“Kama utasema ziko Kenya ziko wapi, tutakuchukua chini ya ulinzi kwenda benki mama, baba umeshinda nyumba lipa. Mnada tutaurudia palepale na asilimia 75 ya yule mshindi atatakiwa kulipa la sivyo fedha aliyotoa awali ya asilimia 25 haitarudishwa,” amesema Kevela.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment