Rais Mugabe kuburuzwa mahakamani

Baada ya kutangaza jana usiku kuwa hataachia madaraka kwa sasa, Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe chama chake cha Zanu-PF  kilichomuweka madarakani kwa miaka 37 kimesema kitamshitaki kiongozi huyo wa zamani wa chama hicho.

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.
Chama cha Zanu PF kupitia mtandao wa Twitter kimeripoti kuwa kitamfungulia kesi Rais Mugabe endapo hatajiuzulu ndani ya muda aliopewa.
Jana kwenye mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Zanu PF, Rais Mugabe alivuliwa nafasi ya kiongozi mkuu wa Chama hicho na kutakiwa ajiuzulu leo kabla ya saa 6 mchana kwenye nafasi ya urais wa taifa hilo.
Taarifa kutoka mtandao wa BBC zinaeleza kuwa  kwenye mazungumzo kati ya Makamanda wa jeshi na Rais Mugabe alikubali kuondoka madarakani , lakini baadae wakati analihutubia taifa akabadili mawazo.
Jeshi linatarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari leo jumatatu asubuhi pamoja na Muungano wa Wapiganaji waliopigania Uhuru wa Zimbabwe.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.