Serikali yamalizia kiporo cha miaka 70 kilichoachwa na Baba wa Taifa

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa watu waliubeza uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma ambayo ni Makao makuu ya nchi.

Dkt. Abbasi amesema hayo jumapili hii, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akitoa tathmini ya miaka miwili ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambapo ameeleza kuwa imepita miongo minne takribani miaka 44 tangu azimio hili lipitishwe na baba wa Taifa.
“Lakini kuna huu uamuzi wa Dodoma serikali kuhamia Dodoma watu waliubeza haiwezi kutokea, ni uamuzi ambao unatokana na azimio la serikali yetu miaka tangu ya 70 imepita, miongo minne takribani miaka 44 tangu azimio hili lipitishwe na baba wa Taifa, kwamba jamani tuazimie kuhamia Dodoma, lakini ndani ya miaka hii miwili ya serikali hii yenye maamuzi magumu lakini makini wote mnajua kwasasa serikali ipo Dodoma,” alisema Dkt Abbas.
“Kwa maana ya Waziri Mkuu, Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote,baadhi ya wakurugenzi kwasababu mwaka huu wengi ndio watamalizika kabisa lakini mmesikiaa Makamu wa Rais wakati wowote mwaka huu atahamia Dodoma na wakati wowote ule mwakani Mh. Rais atahamia Dodoma na mimi niwajulishe rasmi vilevile nimeshahamia Dodoma mkiniona Dar es salaam nipo kikazi maalum kwahiyo agizo hili na azimio ninalolisema hatimae baada ya miaka takribani 40 zaidi sasa tumehamia Dodoma sasa haya ni mafanikio na misimamo ya serikali hii kwamba ikiamua jambo inatekeleza.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment