Spika Ndugai aipa kibano serikali kuhusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameitaka serikali kutoa tamko au taarifa bungeni kuhusu mikopo ya wanafunzi wanaosoma Elimu ya Juu huku akieleza kuwa wanafunzi wengi wa masikini wakizagaa nchi nzima inakuwa ni matatizo.
Akizungumza baada ya Mbunge Mbunge wa Viti Maalum Martha Mrata kuhoji

kuwa kumekuwa na tatizo kubwa wanafunzi wakifika chuoni wanafunzi wa masikini wanafunzi yatima ambao wamefika bado wanakutwa na tatizo kwamba walipe fedha yakusajiliwa pale chuoni tatizo hili limekuwa ni kubwa wanafunzi wamekuwa wengi na sisi wabunge tumeombwa sana nawanafunzi hawa ili tuwalipie fedha za kusajili waweze kuwa wanafunzi pamoja na kwamba wana mkopo, sasa Mh. Spika nilikuwa naomba m,uongozo wako ili serikali iseme ni kitu gani inaweza kufanya kuondoa tatizo hili asante.
“Kuhusu muongozo huu wa Mh. Martha Mrata jambo hili ni serious kabisa, wala sio wa mwaka wa kwanza peke yake na wa miaka mingine, wawe mwaka wa pili mwaka wa tatu yani mtu ana mkopo anatakiwa akifika chuoni alipe kwanza fedha za kuwa registered hapo chuo alafu sasa akishasajiliwa na chuo ndio sasa apate ile haki yake ya mkopo sasa watoto hawa ni wamasikini wanazagaa nchi nzima ni matatizo makubwa,”alisema Spika Ndugai.
“Sasa naomba serikali itoe tamko au taarifa kamili ya kuhusu nini kinachoendelea na kuhusu mtu anadai haki yake hapewi mpaka kuwe na utaratibu atoe tena hela.”a
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment