Ukweli utaniweka huru daima – Katambi

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Mjumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe Kamati ya Maadili Taifa, Patrobass Katambi amesema ukweli utamuweka huru daima,hekima na busara zake ndio zilimlazimisha kuondoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Patrobass akiongea na Bongo5 leo amesema kuwa amekihama chama hicho bila kufafanua yaliyomtoa katika chama hicho ili kuacha haiba yao na waendelee na mfumo wao wa siasa mpya.
Sio kwamba sijawajibu, nimewajibuni kwamba asante kwa maswali yote 8 ila hekima na busara zangu zilinilazimisha kuondoka chadema na kuhamia CCM bila kufafanua yaliyonitoa ili kuacha haiba yao waendelee kwa Amani na mfumo wao wa Siasa mpya.
Ila kwakuwa CHADEMA wamenishambulia kwa UONGO kupitia Viongozi wao Wakuu niliowaheshimu sana, sasa nawapa “reasonable time” Wawathibitishie Watanzania kwa ushahidi in Public.
Ikiwa waliyonituhumu si ya kweli au wakakaa kimya bila kukanusha;

Nitalazimika kuwajibu na kutoa sasa sababu za kuhama kwangu Chadema kupitia ‘Press Conference’ nanyi mtaarikwa.
Acha tuwe wanachama wa kawaida CCM chama cha wanachama kinachoruhusu tushauri,tuwakosoe kwa staha viongozi na kuthamini vijana sio kuua vipaji vyao, kuwaburuza na kuwafanya watumwa katika Ufalme wa Misri ya Farao, kuwasaidia kujenga nchi na kudumisha Amani sio ulaghai, porojo na usanii kama huu wa kutuhumu na kuchafua kila anaeondoka Chadema kwa kutunga kashfa ili kumdharirisha mtu na utu wake bila ushahidi. Huku ni kutoheshimu haki ya kikatiba ya kuingia na Kutoka katika chama.
UKWELI UTANIWEKA HURU DAIMA na nipo tayari kulipa gharama zake hata iwe kifo kwa maslahi ya Taifa na Watuwake” Mungu ibariki Tanzania.
Patrobass Katambi
Mwanachama wa CCM.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment