Wabunifu wa mavazi watakiwa kulipa Kodi

Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) limetoa onyo kali kwa wabunifu wa mavazi ambao wamekuwa wakikwepa jukumu lao na kulipa kodi.


Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua akiwa katika uzinduzi wa msimu wa 10 wa Swahili Fashion Week.
Onyo hilo limetolewa na Afisa Ukuzaji Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Vivian Shalua wakati akizindua msimu wa kumi wa Maonyesho ya Mitindo Tanzania, Swahili Fashion Week.
Vivin alisema, Kuna kundi kubwa la wabunifu ambao hawafuati masharti ya kufanya kazi pamoja na kukwepa kulipa kodi.

“Kwa miaka mingi wabunifu wamekuwa na tabia ya kukwepa kodi, sasa mwisho wao umefika, serikali ya Rais Magufuli haiwezi kufanya kazi na watu ambao hawalipi kodi ndio maana nasema hawa wote watashughulikiwa,” alisema Shalua
Shalua alisema Swahili Fashion ni maonyesho ambayo yamekuwa na mafanikio makubwa sana nchini Tanzania pamoja na Afrika nzima kutokana na kufanyika kwa miaka 10 mfululizo bila kukataka kata.
“Haya maonyesho yamekuwa na mafanikio makubwa sana toka yaanze, kama ulivyosikia tayari kuna wabunifu wengi wamefanikiwa kutokana na haya maonyesho toka aanzishwe imekuwa ni kama platform ambayo imekuwa ikiwatangaza wabunifu na kuwapatia masoko ya kazi zao. Pia nimesikia kuna wabunifu zaidi ya 50 ambao watashiriki, unaona ni namna gani watu wengi wanavyonufaika na mzunguko wa maonyesho haya kwa ujumla,” alisema Shalua.

Mmoja kati ya wabunifu wakitoa zawadi kwa waandishi wa habari
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Maonyesho hayo, Mustafa Hassanali amesema maonyesho ya mwaka huu yatakuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuwa na wabunifu wengi kutoka nchini mbalimbali za Afrika Mashariki.
“Tunawakaribisha sana watanzania katika msimu mpya na wakumi wa Swahili Fashion Week, kama kawaida kuanzia tarehe 1,2,3 tukio litafanyika katika Makumbusho ya Taifa Posta, tunawakaribisha watanzania wote na huo ndio uwanja wetu akujivunia,” alisema Mustafa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment