Wema Sepetu achoshwa na matusi ya mitandaoni ‘Kuna wakati natamani Mungu anichukue’

Malkia wa filamu nchini, Wema Sepetu amechoshwa na maneno machafu ya watu yanayoendelea katika mitandao ya kijamii.

Muigizaji huyo amedai ni bora Mungu aichuke nafsi yake ili aachwe kusemwa kwa mambo machafu pamoja na kutukanwa.

Ipo siku nitakufa, hakuna anaeishi milele. Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo itakuwa“Maskini ya Mungu, Dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze Roho yake mahali pema…”,” aliandika Wema Instagram.

Aliongeza, “Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah wata’allah anichukue tu… Ya Duniya ni mengi sana…. Kuna muda mwingine nakufuru mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge exist… Ila acha niendelee kumtegemea yeye… Kila jambo hutokea kwa sababu…. Hili nalo litapita… I think I need a Time Off Social Media… Kwa mara nyingine Tena…. Siwezi jamani,”

Muigizaji huyo ambaye anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya, siku chache zilizopita alikuwa nchini Rwanda katika shughuli zake za sanaa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment