Wema Sepetu apokelewa kama Malkia nchini Rwanda, aeleza kilichompelekaMsanii maarufu wa Filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu jana jumatano usiku aliwasili nchini Rwanda ambako alieleza kuwa ameenda kikazi kwenye Tamasha la KFM Instagram Party.

Wema Sepetu kwenye mkutano na Waandishi wa Habari jijini Kigali.
Wema Sepetu amesema ameenda nchini Rwanda kwa ajili ya tamasha la KFM Instagram Party, Tamasha linaloandaliwa na kituo cha Radio cha KFM lenye lengo la kuwakutanisha watumiaji wa mtandao wa Instagram nchini humo, na litafanyika Novemba 24, 2017, katika ukumbi wa Chillax Lounge, Nyarutarama jijini Kigali.

Ndio mara yangu ya kwanza nimekuja (Rwanda) ndege imegusa ardhi saa mbili na nusu naweza kusema sina hata lisaa tangia nimefika, vile nimekuwa nikisikia kuhusu Rwanda nimeviona, najua bado ni usiku kesho nitaweza kuona mengi zaidi, nimesikia kwamba Rwanda ni nchi ambayo ni ndogo lakini ni nzuri, nilikuwa niko na kaka yangu tunapisha barabarani napigwa na butwaa ‘oh my God hii sehemu ina usafi mwingi.”amesema Wema Sepetu kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mapema jana usiku baada ya kuwasili nchini Rwanda na kueleza kilichompeleka.

Ni jambo jema kwamba nimekuwa Queen of Social Media, siyo kwamba nimejipa mwenyewe, watu wamenipa hicho cheo, naamini itakuwa ni muda mwafaka wa watu kukutana nami ana kwa ana, kwa sababu kuonana kwenye ‘ma-social media’ tu mtu anakuwa anatamani kukuona, eti huyu Wema natamani nikae naye nipige naye picha, tupige naye stori mbili tatu, sitaweza kufanya hivyo na watu wote ila angalau watu waweze kupata taswira halisi kuhusu mimi kipenzi cha wengi kutoka Tanzania. Mimi ni mcheshi, napenda burudani napenda matamasha naamini nitafurahi kuwa na watu wangu wa Rwanda hasa ukizingatia huu mwaka unaelekea ukingoni, 2017 ni mwaka ambao kwangu mimi umekuwa ni mrefu sana, pia nashukuru Mungu unaisha.”amesema Wema Sepetu.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment