Baada ya Mbunge wa CHADEMA kutangaza kuhamia CCM, Mhe. Lema aeleza wanavyorubuniwa

Baada ya Mbunge wa jimbo la Siha kupitia tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel leo kutangaza kujivua Ubunge na kuhamia CCM. Mbunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema ametaja marupurupu na vitu ambavyo wabunge kutoka vyama vya upinzani wanavyorubuniwa.

Mhe. Lema ametaja vitu hivyo ikiwa ni masaa machache baada ya Mhe. Mollel kutangaza kujivua nafasi hiyo ya Ubunge.
Nitakupa mshahara wako wote kwa miaka iliyobaki,pia nitakulipia madeni yako yote,nitakupa kiinua mgongo chako chote nitakupa na mlinzi kwa kipindi hiki na ukitaka tena kugombea nitakupa kipaumbele wewe au kazi nyingine utakayotaka ? Je,utakuwa tayari?Si utakuwa tiyari wajameni?.“ameandika Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Awali kulivuma tetesi kuwa Mhe. Lema naye ni moja ya Wabunge wa Vyama vya Upinzani wanaotarajiwa kujiunga na CCM baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuweka picha akiwa na Lema na kuandika maneno yaliyoleta utata.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment