Jibu la Mwana FA kuhusu ujio wa kolabo na Lady Jaydee

Baada ya kumaliza tofauti zao hivi karibuni kisha kuonekana wakiwa studio pamoja, hatimaye Mwana FA amefunguka iwepo kuna kolabo kati yake na Lady Jaydee.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Hata Sielewi’ katika mahojiano na Planet Bongo, EA Radio amesema bado ni mapema kusema moja kwa moja kuna kazi inakuja kwani ndio wametoka kumaliza tofauti zao ila kadiri muda unavyozidi kwenda kuna uwezekano wa kufanya tena kazi.
“Sehemu ya kwanza ya hiki kitu kulikuwa na tofauti na sehemu kwanza kulikuwa ni kumaliza tofauti zetu katika level ya urafiki/kiubinadamu kwanza halafu vitu vingine vyote vitafuata kama kuna uwezekano wa kufanya, kama ni muziki utafanyika na kama hakuna a least sisi kama binadamu kama marafiki tuko sawa” amesema.
“Hivyo muziki utafanyika au hapana ipe time kidogo, msije watu mkaondoa tofauti hapo hapo mnataka mfanyi muziki maana yake mmeondoa tofauti ili mfanye muziki nafikiri tuiweke kwenye level ya kiubinadamu kwanza halafu kama kuna lolote lifuate” ameongeza Mwana FA.
Lady Jaydee na Mwana FA wameshaweza kutoa hit songs kama Hawajui, Msiache Kuongea, Alikufa kwa Ngoma, Wanaume Kama Mabinti na Sitoamka bila kusahau ngoma walioshirikishwa na Ngwea ‘Sikiliza’
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.