Kauli ya RC Makonda kwa Wema Sepetu

Baada ya Wema Sepetu kutangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuanzia mwishoni mwa weekend iliyopita ameonekana akiwa katika picha tofauti tofauti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda.

Sasa leo RC Makonda ameandika ujumbe kwa kwenye moja ya picha walizopiga pamoja. Kupitia ukurasa wake wa Instagram RC Makonda ameeleza kuwa Wema amechagua fungu jema katika maamuzi aliyofanya.
Serikali ni sawa na Mzazi ambaye siku zote huwaza mema kwa watu wake. Umechagua fungu jema karibu nyumbani tujenge Nchi imara na wala siyo upinzani imara kwani Nchi kwanza vyama baadae
Kabla ya RC Makonda, Wema naye aliandika; “I never knew you well until I hated you, & now that I met you, I thank God to have Found you… Every Dark Cloud possesses a Silver Lining”.
February 24 mwaka huu Wema alijiunga na Chadema akitokea CCM na December Mosi akatangaza kurejea CCM.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment