Mabaya mengi yamefanya nimejulikana – Gigy Money

Msanii wa muziki Bongo, Gigy Money amesema matendo yake mengi mabaya ndio yamepelekea watu kumjua.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Papa’ ameimbia E-Newz ya EATV kuwa licha ya mabaya yake kupelekea kujulikana ila watu wamempenda kutokana na mema anayofanya.
“Mabaya mengi yamefanya nimejulikana ila kupendwa kwangu siyo kwa mabaya bali mema yangu ndio maana watu wananipenda”
amesema Gigy Money.

Pia ameongeza kuwa watu wampende Gigy Money kwa mema yake na mazuri ila mabaya wamuachie kwa sababu hata yeye anajaribu kuyapotezea.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment