RC Gambo awavuruga CHADEMA, Adai Mhe. Lema yupo mbioni kujiunga CCM

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewavuruga wanachama wa Chadema baada ya kuweka picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na kuandika kuwa Lema yupo mbioni kurudi nyumbani.
Maneno aliyoambatanisha RC Gambo na picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram yalisomeka “Msituko yupo mbioni kurudi nyumbani!” jambo ambalo liliibua utata kwa baadhi ya wafuasi wa Chadema.

Hata hivyo mpaka sasa Mhe. Lema hajaongea chochote kuhusu kauli hiyo ya RC Gambo. Je, kwa maoni yako unadhani Lema anaweza kuungana na CCM kama alivyofanya aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CUF, Maulid Mtulia. ?
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment