RC Kilimanjaro, Mhe. Anna Mgwira ahamia CCM

Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro, Mhe. Anna Mgwira amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) akitokea Chama cha ACT Wazalendo.
Mhe. RC Mgwira aliwahi kuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo kabla ya kuteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa na kuachana na nafasi hiyo ndani ya chama hicho na mwanachama wa kawaida.
Mhe. RC Mgwira ametangaza uamuzi huo leo hii wakati wa Mkutano Mkuu wa UWT uliofanyika mjini Dodoma ambapo amesema baada ya kujitakari kwa muda na kufanya kazi na serikali ameona ni muda muhafaka kutamka kuwa anahamia CCM.
“Kwa muda mfupi nimeiona CCM inayobadilika, nimeona juhudi za kila mtu, ninaiona CCM inayoanza kukataa rushwa, nimeiona CCM inayoanza kulipeleka taifa letu mbele” amesema Mhe. RC Mgwirwa
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment