Aliyefungwa miaka 60 aongezea mingine 175 kwa ukatili wa kingono

Aliyekuwa daktari wa timu ya Olimpiki nchini Marekani, Larry Nasser amehukumiwa kwenda jela miaka 175 baada ya kukutwa na makosa ya ukatili wa kingono dhidi wananawake na wana michezo.

Wakati hukumu hiyo ikitoka Larry Nasser alikuwa tayari akitumikia kifungo cha miaka 60 kutokana na kukutwa na hatia ya kumiliki picha ngono za watoto kinyume cha sheria.
Jaji Rosemary Aquilina ameiambia mahakama kuwa amejisikia fahari na furaha kubwa kutoa adhabu hiyo kutokana na kitendo alichofanya Nasser na kwamba anataka iwe fundisho kwa wengine.
Takriban wasichana 140 wamewasilisha kesi dhidi ya Nassar, taasisi ya USA Gymnastics na chuo kikuu cha MSU, wakidai kuwa taasisi hizo mbili zilipokea tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya daktarihuyo miaka kadhaa ya nyuma.
Taasisi hiyo ya michezo na chuo hicho zimekana kuwa kulikuwa na chochote cha kufichwa.
Hukumu ya Larry Naser inafuatia wiki ya ushuhuda kutoka kwa wanawake takribani 160, wakiwemo washindi wa medali ya dhahabu ya olympiki Biles, Aly Raisman, Gabby Douglas na McKayla Maroney
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment