Asilimia kubwa wanaoweka picha chafu mitandaoni sio wasanii – Batuli

Msanii wa filamu, Batuli amefunguka kwa kudai kuwa tasnia ya filamu na muziki inachafuliwa na watu ambao wanajifanya wao ni wasanii kumbe sio.

Muigizaji huyo amesema hayo baada ya Naibu Waziri wa Habari,Juliana Shonza kumtaka Gigy Money kuripoti ofisi kwake kutokana na kupiga picha za nusu uchi huku mwanadada Pretty Kind anayedaiwa kuwa ni msanii wa filamu akifungiwa miezi 6 kujihusisha na kazi za sanaa.

“Asilimia kubwa ya wanaotupia picha chafu kwenye mitandao hawapo kwenye makundi haya mawili muziki na filamu, umaarufu wao wameupata kwa kupiga picha za utupu na kuzitupia kwenye mitandao ya kijamii na watanzania wasio na maadili kuwapokea kwa shangwe #SanaaIpeweHeshimaYake,” alisema Batut
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.