Baada ya Mahakama kutoa hukumu kwa ‘Scorpion’, Aliyetobolewa macho afunguka mazito

Baada ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo Januari 22, 2018, kumuhukumu, Salum Njete maarufu kama ‘Scorpion’ aliyekuwa akituhumiwa kumchoma kisu na kumtoboa macho, Saidi Mrisho kwa adhabu ya kwenda jela miaka saba na kulipa fidia ya shilingi milioni 30 kwa kosa la kujeruhi na wizi, hatimaye muhusika aliyefanyiwa ukatili huo apingana na hukumu ya Mahakama kwa kudai amepewa adhabu ndogo.

Said Mrisho
Saidi Mrisho ambaye alifanyiwa tukio hilo la kinyama amefunguka na kusema kuwa hajaridhika na maamuzi ya mahakama hiyo na kudai kuwa mtuhumiwa huyo ‘Scorpion’ alikuwa anastahili kufungwa maisha jela au na yeye angetobolewa macho kwa kuwa yeye sasa hivi anaishi maisha magumu yasiyoelezeka.
Hukumu hii imeniumiza sana, kwa sababu tayari ameshaniharibia maisha nina familia na nina watoto, Watoto wangu wanasoma  sasa inabidi watoto wangu niwahamishie shule za serikali, kwa sababu sina pesa na maisha ninayoishi ni ya kupanga kwa sababu sina nyumba na nyumba niliyoahidiwa sikupewa. Kwahiyo sasa mtu ambaye anakuharibia maisha, alikuwa anataka kupoteza malengo yangu, anafungwa miaka 7 na hiyo faini ya milioni 30. Kwa familia niliyonayo hiyo milioni 30 ni ndogo na hiyo hukumu ya miaka saba ni ndogo sana. Kwa hiyo inaniumiza sana na watoto wangu,“amesema Mrisho huku akibubujikwa na machozi ya hudhuni mapema baada ya Mahakama kutoa hukumu huku akieleza dhamira yake ya kutaka kuonana na RC Makonda na Rais Magufuli.
Kwa hili hapa mimi linaniumiza sana , nitaomba nitafika kwa Mkuu wa Mkoa, na nitaomba nifike kwa Mhe. Rais nampenda sana na anajitihada kubwa sana kwa Wananchi wake nitaomba anisaidie kwa hili,“amesema Mrisho.
Katika hali isiyo ya kawaida, mnamo mwezi Septemba mwaka 2016 maeneo ya Buguruni Kwamnyamani, Said Mrisho akiwa maeneo hayo majira ya usiku alivamiwa, akaporwa vitu, akajeruhiwa tumboni na kutobolewa macho yake yote mawili tukio lililopelekea Mrisho kupatwa na upofu wa milele.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment