Diamond ashindwa kuvumilia yanayoendelea kuhusu yeye na Wema

Picha na video ambazo zimesambaa mtandaoni zikimuonyesha Wema Sepetu akiwa karibu na Diamond Platnumz katika party ya kumkaribisha Maromboso ‘Mbosso’ iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam zimeibua mambo mengi.

Mashabiki wa Diamond walionekana kupingana na bosi huyo wa WCB baada ya kuonekana kumkaribisha Wema Sepetu kwenye tukio hilo kitu ambacho Diamond amepingana nacho.
“Wengi hupenda kuona watu wakiwa wana Vita ama uhasimu usio na kichwa wala miguu… Eti utamsikia mtu anasema “Dogo Mi shabiki yako Mkubwa na nakukubali sana ila kitendo cha kumualika Wema Umeniuzi,” aliandika Wema Instagram.
Aliongeza, “Kwa hiyo we unataka mie niendelee kuwa na vita ama niwe na vita na Wema ili iweje? yani mie nikiwa na vita na Wema we unafaidika nini? na itanisaidia ama kusaidia nini kwenye Sanaa yetu? Huwezi kuwa shabiki yangu halaf unafurahia mie kuendelea kuwa na vita na mtu, tena vita ambayo imeshaisha…nina familia yangu Naipenda Naiheshimu na siwezi kuiacha… ila hio sio sababu ya kuwa na vita na watu…na huu ni mfano wa kwanza mwingine unafata…. Huu sio Muda wa kujenga chuki zisizo za msingi ni wakati wa wasanii kushirikiana na kwa pamoja kufanya kazi na kukuza sanaa zetu kwajili ya future ya wadogo na vizazi vyetu vijavyo… Shukran sana Mdam kwakuja usiku wa jana…Mwenyez Mungu akubariki na akujalie kila la kheri uliombalo….. #Watakubali by @Mbosso_ link in his and my BIO,”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.