Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ afikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya uchochezi

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo amefika katika mahakama kuu Kanda ya Mbeya akituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi.

Mwingine aliyefikishwa mahakani hapo ni Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga ambaye naye anakabiliwa na mashtaka sawa na Sugu.
Hapo jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram aliandika; ‘polisi wameniita  wanipeleke mahakamani kwa wanachodai ni ‘Uchochezi’ najiskia kama Nyerere wakati wa Ukoloni au Mandela wakati wa Ukaburu, Siogopi na msiogope’.
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Emmanuel Masonga wanadaiwa kutoa maneno yenye kuleta chuki baina ya wananchi na serikali katika mkutano walioufanya December 30 mwaka jana.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment