Juma Nyoso mikononi mwa polisi kwa kumtwanga shabiki

Beki wa Kagera Sugar Juma Nyoso amejikuta akitiwa mbaroni na polisi mjini Bukoba kwa madai ya kumtwanga shabiki ngumi mara baada ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Kagera Sugar kupigwa 2-0 na Simba SC kwenye dimba la Kaitaba.


Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya mpira kumalizika wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo (dressing-room) ambapo inadaiwa kuwa baadhi ya mashabiki wanaoaminika kuwa ni wa Kagera Sugar wakawa wanawarushia maneno makali (matusi) wachezaji hao.
Kufuatia maneno hayo, Nyoso alionekana kukosa uvumilivu na kuamua kumtwanga ngumi mmoja wa mashabiki hao ambaye alizimia papo hapo.
Gari ya wagonjwa (ambulance) ilifika na kumchukua majeruhi na kumkimbiza hospitali na dakika chache baadaye polisi walikwenda kumchukua Nyosso na kwenda naye kituo cha polisi..
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.