Naweza kuandamana au kufanya chochote kisa Mhe Sugu – Faiza Ally

Mwanadada Faiza Ally ambaye pia ni mzazi mwenza na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu ameibuka kwa kudai kwamba anaweza kufanya chochote kwaajili ya mzazi mwenzake huyo.

Mh.Sugu Mbilinyi aliburuzwa kotini Alhamisi hii kwa kosa la kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi.

Faiza Ally ameibuka kumkingia kifua mzazi mwenzie huyo kwa kusema ikibidi ataandamana ili Baba Sasha apate haki yake.

“Just to let you know guys: kamwe sitaweza hata siku moja kufurahia matatizo ya baba Sasha kufurahia matatizo za baba Sasha hata ikibidi kuandamana apate haki yake ningefanya hivyo!
Matatizo yangu na yeye ni mapenzi tu na si vinginevyo na yaliisha! Mwisho wa siku ni baba wa mwanangu na wanapendana sana na mwanae wamefanana mpaka harufu zao kila ninapomuona namuona baba yake na nikifanya ubaya ntakuwa namfanyia mwanangu,” aliandika Faiza Ally kupitia Instagram.

Aliongeza, “All I wish Sasha na baba yake wawe hai, wawe na furaha siku moja niwaone wako pamoja happy and success. So kama mnahisi nafurahia mpo wrong na kwa kifupi nimetafutwa na watu wengi, wa siasa na wanamuziki ili nimchafue au nishirikiane nao lakini sijawahi kuwapa nafasi. Nikiwasha MOTO wangu ni wa sababu zangu binafsi na siyo kutumiwa and by the way amelipa ada ya Sasha and hope in future atakuwa baba bora zaidi kama alivyo mwanzo. Na ninamuombea heri Mungu amfanyie wepesi na amuonyeshe njia pasipo kuwa na njia!” ameandika Faiza.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment