Neno la Babu Tale kwa mume wa Shilole, ‘Mkigombania chumbani njoo kwangu’

Meneja wa WCB na Tip Top Connection, Babu Tale ambaye alikuwa msimamizi wa ndoa kati ya Shilole na Uchebe, amewataka pindi wanapopishana katika ndoa yao kutopeleka mambo hayo katika mitandao ya kijamii.

Tale amesema endapo watafanya hivyo wasifike kwake ila kama ugomvi utakuwa wa ndani kwa ndani wasisite kufika wake.
“Kama unampenda usigombane naye kwenye mitandao, kwa hiyo kama mnagombana na mpenzi wako mnaenda kugombania Instagram, mtaachana na kwangu usije,” Tale amemueleza Uchebe.
“Kama mkigombania chumbani njoo kwangu any time tutayamaliza, kama mnagombania kwenye mitandao hayo si mapenzi,” amesisitiza.
Hata hivyo amesema si kwamba anamkataza kujidai na mkewe katika mitandao ila anapaswa kutambua kuwa amezungukwa na mbwa mwitu ambao kazi yao ni kuharibu maendeleo ya ndoa za watu.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment