Ninakwenda bungeni kulia – Mgombea ubunge kupitia CHADEMA

Mgombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CHADEMA, Salum Mwalimu amesema kuwa akifanikiwa kuchukua jimbo hilo basi atakuwa mwendawazimu bungeni katika kutetea maslahi ya wananchi wake.

Salum Mwalimu 
Mwalimu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar amedai kuwa jimbo hilo limekuwa nyuma kimaendeleo kitu ambacho kimeondoa hadhi yake pamoja na watu wake na kuahidi kuwa atapigania kwa hali na mali kuweza kurudisha heshima ya jimbo hilo kwa kulilia vitu muhimu serikalini ili kurudisha hadhi ya Kinondoni.
Ninakwenda bungeni kulia, ninakwenda bungeni kuwa mwendawazimu kwa ajili ya mahitaji ya watu wa Kinondoni,“amesema Salum Mwalimu jana kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari.
Hata hivyo, Mwalimu amesema kuwa jimbo hilo linachangamoto nyingi ikiwemo ubovu wa miundo mbinu, Changamoto za huduma ya Afya na kuahidi kuwa kero hizo zitakwisha kwani yupo tayari kupigania maslahi ya watu wa Kinondoni.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.