Sitokuja kutoa ngoma kubwa kama Hainaga Ushemeji – Man Fongo

Msanii wa muziki wa Singeli Bongo, Man Fongo amesema katika maisha yake ya muziki hatokuja kutoa ngoma kubwa kama Hainaga Ushemeji.

Muimbaji huyo ambaye anatamba na ngoma yake mpya ‘Lau Nafasi’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa ngoma hiyo ndio ilifungua milango kwa muziki wa singeli hivyo ni vigumu kuishusha.
“Ile Hainaga Ushemeji ni official kutambulisha muziki wa singeli na kuwaelekeza watu kuna muziki unaitwa kisingeli na sitaokuja kutoa ngoma kubwa kama hainaga ushemeji,” amesema Man Fongo.
Ameongeza kuwa kwa sasa wasanii wengine wanapata fedha nyingi kutokana na ngoma hiyo hiyo ku-hit kitu ambacho sasa kushika milioni mbili hadi tatu ni jambo la kawaida.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment