Wakili msomi Alberto Msando ampa ushauri Lemutuz ‘hakuna kosa kuwa na kibamia

Wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii kulivuja video ambayo ilikuwa inamuonesha Mjasiriamali na mtu maarufu mitandaoni, Lemutuz akiwa utupu hatimaye Wakili Msomi Alberto Msando ametoa neno akimshauri jambo la kufanya katika kipindi hiki kigumu kwake.

Lemutuz na Alberto Msando
Wakili Msando amesema kuwa tatizo sio kuonekana akiwa uchi bali tatizo linakuja pale watu wanavyotumia nafasi hiyo kumdhalilisha na kumdhihaki huku akimtaka Lemutuz akae kimya kwani ndio suluhisho pekee lililobakia.
Ushauri wangu (unaweza ukawa wa kipuuzi na usio na maana) ni mwepesi. Endelea na maisha yako. Pambana kuijenga Le Mutuz TV. Endelea kuelimisha na Straight Talks zako. Endelea kufurahia maisha. Usijibizane na wanaokutukana. Usiwashambulie wanaendelea kukudhalilisha. Fanya yale yanayokupendeza na kukufanya uwe bora zaidi. Na zaidi ya yote jifunze kutokana na hili.“ameandika Alberto Msando kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Kwa upande mwingine Msando amesema tatizo sio kuwa na Kibamia (Tafsiri ya Kibamia ni uume mdogo) kwani kwenye jamii yetu wapo watu wengi wanaishi na vibamia ila amechukizwa na jinsi watu wanavyomshambulia.
Kosa sio ‘kibamia’ au kujifuta ulipotoka kuoga. Wengi sana wana ‘vibamia’ na wanaoga na kujifuta. Wengi wamekutana navyo na wanaishi navyo. Wala hakuna kosa kuwa na kibamia. Utu na heshima yako ni zaidi ya kila kitu. Ni huzuni kwamba unadhihakiwa, unadhalilishwa kwa sababu hiyo. Haya ndio mambo wengi wanayapenda na kufurahia,“ameandika Msando.
Soma ushauri wote wa Alberto Msando kwa Lemutuz hapa chini;
Kaka na rafiki yangu @lemutuz_superbrandtz; Nimetamani sana nikae kimya upambane na ‘msala’ wako mwenyewe. Lakini nimeshindwa. Nimeshindwa kwa sababu naelewa na najua inavyokuwa pale unapopitia unachopitia. I have been there.
Niseme kwamba kwa comments zote unaweza sasa kuelewa kiasi cha chuki dhidi yako. Kiasi cha furaha kwa maadui zako. Lakini ndani yake usiache kuona kiasi kidogo cha upendo na huzuni kutoka kwa marafiki zako.
Kosa lako ni kuruhusu kile ambacho wengi wanafanya kufika hadharani kwa kuwa karibu na kumpa nafasi aliyefikisha. Hilo ndio kosa lako la kwanza. “Kosa” la pili ni unavyoishi. Umeamua kuishi maisha yako vile ambavyo wewe mwenyewe umechagua. Kuna wengi wanakereka bila hata sababu. Ni maisha yako!
Kosa sio ‘kibamia’ au kujifuta ulipotoka kuoga. Wengi sana wana ‘vibamia’ na wanaoga na kujifuta. Wengi wamekutana navyo na wanaishi navyo. Wala hakuna kosa kuwa na kibamia. Utu na heshima yako ni zaidi ya kila kitu. Ni huzuni kwamba unadhihakiwa, unadhalilishwa kwa sababu hiyo. HAYA NDIO MAMBO WENGI WANAYAPENDA NA KUFURAHIA. Sad.
Ushauri wangu (unaweza ukawa wa kipuuzi na usio na maana) ni mwepesi. Endelea na maisha yako. Pambana kuijenga Le Mutuz TV. Endelea kuelimisha na Straight Talks zako. Endelea kufurahia maisha. Usijibizane na wanaokutukana. Usiwashambulie wanaendelea kukudhalilisha. Fanya yale yanayokupendeza na kukufanya uwe bora zaidi.
Na zaidi ya yote JIFUNZE kutokana na hili.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment