Ajali ya barabarani yaua watano Tanga

Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine sita kujeruhiwa vibaya, baada ya basi kampuni ya AJ Safari kugongana na Toyota Hiace katika eneo la Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga.

Akithibitisha vifo hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Leonce Rwegasira amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 5:30 asubuhi huku akieleza chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa kutozingatia sheria za barabara.

Alitaja namba za magari yaliyohusika katika ajali hiyo, ACP Rwegasira amesema ni basi la Kampuni ya AJ Safari lililokuwa likitoka Lushoto kwenda Dar es Salaam likiendeshwa na Khalifa Mussa Omary mkazi wa Chamanzi Dar es Salaam lenye namba za usajili T 497 BJB mbalo limegongana na Hiace iliyokuwa ikitoka Mkata kwenda Segera yenye namba T591 AKE.
Akiwataja waliofariki kwenye ajali hiyo, ni dereva wa Hiace aliyefahamika kwa jina moja la Shabaan, wengine majina yao hayajatambulika na maiti zao zimehifadhiwa Kwenye Hospitali ya Magunga wilayani Korogwe huku majeruhi wakiwahishwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment