Chama cha Mitindo ‘FAT’ chazinduliwa Tanzania

Baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) miezi mitatu iliyopita, kutaka wabunifu nchini kuanzisha chama kitachowakutanisha pamoja katika shughuli zao, leo Januari 31, Chama cha Mitindo Tanzania (FAT) kimezinduliwa rasmi.

Akizindua chama hicho, Katibu Mtendaji Basata, Godfrey Mngereza amesema uanzishwaji wake licha ya kuwainua wabunifu wachanga na wakubwa kutambulika kimataifa, utakuza viwanda vya pamba na ngozi nchini ambavyo vitategemea malighafi za ndani.
Mngereza amesema wabunifu wakijengewa utamaduni wa kutumia bidhaa za ndani kama ngozi na nguo kutengeneza mavazi yenye utamaduni wa ndani, wataendana na kauli ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya viwanda. Mngereza amesema Serikali inafanya kazi na chama kinachotambulika kisheria kikiwa kimesajiliwa hivyo kupitia chama hicho wataweza kuelekeza matatizo yao.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi (TAFCA), Adrian Nyangamalle amesema watahakikisha wanawasaidia katika changamoto mbalimbali zitakazotokea katika chama hicho.
“Tutatoa ushirikiano sehemu yoyote inayohitajika kuisukuma Serikali ili malengo ya chama hiki yatimie kwa haraka,” amesema Nyangamalle.
Mwanzilihi wa FAT, Asia Idarous amesema wamekuwa na changamoto mbalimbali katika tasnia hiyo, hivyo wanaishukuru Serikali kwa kutaka kuanzisha chama hicho kitakachowaunganisha na Serikali ili kuifikisha Sanaa hiyo kimataifa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment