Idris amtaka Diamond kumpigia magoti Zari

Wakati drama zikiendelea baada ya Zari the Boss Lady kutangaza kuvunja mahusiano yake na Diamond Platnumz, Idris Sultani hajakaa kimya huhusu hilo.

Mchekeshaji huyo amemkumbusha Diamond kutekeleza ahadi yake kumpigia Zari magoti kumuomba msamaha kama alivyowahi kueleza hapo awali. Kupitia Instagram yake Idris ameandika;
Wabongo wanafki sana, utasikia “Idris siku ile white party 2015 ndio alimchomea mwana alipomuambia Zari “Embu muone jamaa wako anavyokumbatia fans wake mi nakuambia hata hiyo mimba uliyobeba sio yako lazima ni ya demu mwingine, kakudanganya.
By the way shem ninaanzisha kilimo cha black roses unataka shares ?” Mond naomba tupige yale magoti tuliahidi mpaka sauzi, unashindwaje kumganda wakati Mganda.

 Mwaka jana wakati Diamond akikiri kuzaa na Hamisa Mobetto alisema licha ya kutenda kosa hilo hawezi kumuacha Zari na yupo tayari kupiga magoti kutoka Bongo hadi Afrika Kusini alipokuwa Zari kumuomba msamaha.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment