Kosa la mwaka 2014 lamfikisha Mh. Nassari kortini

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amefi kishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, kujibu shitaka la kushambulia.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Fortunatus Muhalila, alisema mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Jasmine Abdul kuwa, Nassari alimshambulia Neeman Ngudu , Desemba 14, mwaka 2014.
Alisema mbunge huyo alitenda kosa hilo wakati akijua ni kinyume cha sheria. Aidha, Mwendesha Mashitaka Muhalila alisema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na akaomba kupangiwa siku nyingine ili kutajwa kwa shitaka hilo.
Mbunge Nassari ambaye anatetewa na Wakili Sheck Mfinanga, alikana kutenda kosa hilo. Hakimu Abdul aliahirisha kesi hiyo, hadi Machi 6, mwaka huu itakapotajwa tena.
Chanzo; HabariLeo
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment