Mbunge Lema amtembelea Sugu gerezani Mbeya

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amemtembelea gerezani na kuongea na mbunge mwenzake wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na kuongea na mama yake mzazi.

Nimepata fursa leo ya kuongea na Mh Sugu Gerezani pamoja na Mama yake Mzazi nyumbani kwake.Wote wana nguvu na matumaini makubwa,” aliandika Lema kupitia ukurasa ukurasa wake wa Twitter.
Lema alivyokutana na Mama yake Sugu alisema kuwa “Mama sasa wewe unasikitika nini, wewe ni mama wa shujaa unalia nini? Kweli jela ni kubaya, lakini si kubaya kama umekwenda kwa sababu za kupigania haki za wananchi. Sugu hajaua, hajaiba televisheni wala hajabaka, hivyo mama wewe hapa inuka tembea kifua mbele kwamba mwanao yupo gerezani kwa sababu anatetea haki za wananchi, hii ni heshima kubwa sana mama yangu,” alisema Lema.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment