Mchunguzi wa biashara haramu ya meno ya tembo auwawa kikatili

Mwanaharakati na mchunguzi wa biashara ya meno ya tembo duniani, Esmond Bradley-Martin ameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu shingoni akiwa nyumbani kwake jijini Nairobi, Kenya.


Esmond Bradley-Martin
Bradley-Martin (75) alikuwa mpambanaji na mchunguzi wa biashara haramu ya pembe za ndovu na meno ya vifaru duniani.
Tayari Jeshi la polisi nchini Kenya kupitia kwa Mkurugenzi wa Upelelezi jijini Nairobi, Ireri Kamwende amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa upelelezi unaendelea.
Hata hivyo, taarifa hiyo pia imeligusa Shirika la ‘Save Rhino’ juu ya kifo hicho cha mpambanaji.


Bradley-Martin enzi za uhai wake alishawahi kutoa ripoti mbalimbali za kiuchunguzi juu ya biashara hiyo inavyofanyika nchini Kenya hadi nyara hizo zinavyosafirishwa kwenda China na Vietnam ambapo alitaja nchi hizo kama vitovu vya biashara hiyo.
Tukio hilo linajili ikiwa ni mwezi mmoja tu umepita tangu auawe Mwanaharakati mwingine wa kuzuia biashara hiyo ya meno ya tembo ‘Wayne Lotter’ nchini Tanzania.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment