Sheikh Mkuu DAR amtangazia kiama Mange Kimambi ‘hata tumia tena mikono yake’

Baada ya mwanamke maarufu mitandaoni, Mange Kimambi kuposti picha ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhadi Mussa Salim akiwa kwenye picha ya pamoja na makada wa CCM huku akimtuhumu kujihusisha na kampeni za uchaguzi wa ubunge kwenye jimbo la Kinondoni. Hatimaye Sheikh Salim atolea maelezo picha hiyo na kumtangazia kiama Mange Kimambi.
Sheikh Mkuu Dar es salaam, Alhadi Mussa Salim wa kwanza kulia kwenye picha iliyoleta mgogoro.
Sheikh Salim amesema kuwa picha hiyo iliyosambazwa haikupigwa kwenye kampeni bali ilipigwa wakiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail katika eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam ambapo walikutana na Wagombea wawili wa Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kwenye tukio hilo.
Sheikh amesema baada ya kukutana na Wagombea wawili wa CUF na CCM alikaribishwa kuongea na ndipo picha hiyo ilipigwa na nililikuwa ni tukio la kawaida.
Mange Kimambi amekuwa akitukana sana kwenye instagram, amenitukana sana na mbaya zaidi amefika mahala anawatukana mpaka Waislamu, Mange amekuwa jasiri sana kwamba mdomo wake ni mchafu na anataka watu wamuogope kwa mdomo wake mchafu,“amesema Sheikh Salim huku akitangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana mitandaoni.
Sasa kitendo alichokifanya tunataka tumwambie na sauti hii hataisikia tena baada ya leo hatutamjibu na leo sipo hapa kumjibu, ila ninachotaka kusema kwamba ulimi wake aliompa Mwenyezi Mungu anautumia vibaya,  Mikono yake aliyompa Mwenyezi Mungu anaitumia vibaya kudhulumu watu, anadhulumu heshima za watu, sasa mwaka huu ni mwaka wake wa mwisho baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi wake wala mikono yake kumtukana mtu, kwa nini nasema hivi? amejihalalishia mwenyewe maangamizi,“amesema Sheikh Salim.
Akifafanua kuhusu hatua watakayofanya, Sheikh Salim amesema atamshitakia kwenye mahakama ya mbinguni kuhoji kwa Mwenyezi Mungu kama alimpa Mange Kimambi Mikono na ulimi kwa ajili ya kutukana na kuvunja heshima za watu duniani.
Hata hivyo, Sheikh Salim amesititiza kuwa  huu ndio mwaka wake wa mwisho kutukana watu mitandao hususani viongozi wa dini na kudai kuwa tamko lake sio kitisho ni la kweli.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment