Siwezi kufanya kazi na mtu kama sijaendana naye – Rosa Ree

Msanii wa muziki Rosa Ree amesema ni vigumu kwa yeye kufanya kazi na msanii endapo haendani naye.

Rapper huyo anayetamba na ngoma yake mpya ‘Marathon’ amesema hayo wakati akieleza sababu ya kumshirikisha Bill Nass katika ngoma hiyo.
“Bill Nass kabisa ni mshakaji wangu, ni mtu ambaye tuna-vibe pamoja sana as person yeye ni poa sana na mimi napenda watu ambao wapo OG, cha pili mimi siwezi kufanya kazi na mtu ambaye sina vibe naye, mtu ambaye hana positive vibe,” Rosa Ree ameiambia Bongo5.
Ameongeza kuwa kuzaliwa kwa ngoma hiyo kulitokana na idea aliyokuwa nayo hapo awali na Bill Nass alipokuja na yake ikawa kazi rahisi kuikamilisha.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment