So Sad Young Killer na Miss Hip Hop ndio basi tena

Baada ya muda mrefu kutoonekana pamoja, hatimaye msanii Young Killer ameweka wazi kilichotokea kati yake na aliyekuwa mpenzi wake ‘Miss Hip Hop’.

Rapper huyo anayetamba na ngoma ‘Toto Tundu’ ameiambia Clouds Fm kuwa ni kipindi cha miezi sita sasa tangu waachane.
“Kulikuwa na kutoelewana kidogo hatuko pamoja sasa hivi kama miezi sita,” amesema Young Killer.
Hata hivyo ameongeza kuwa si usaliti uliopelekea kuvunjika kwa mahusiano yao kwani hicho ni kitu cha kawaida bali kilichowaachanisha ni sababu za ndani zaidi.
Mwaka 2016  Young Killer alitangaza kumuoa mrembo huyo aliyempa jina la Miss Hip Hip na kila mara wote walipenda kujiachia katika mitandao ya kijamii ila sasa ndio hivyo kila mmoja na maisha yake.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment