Sugu kaniambia niwaambie msiogope – Professor Jay

Baada ya Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Professor Jay) kwenda Mahakamani kusikiliza kesi inayomkabili Mbunge wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), Mbunge huyo amesema kuwa Sugu amesema kuwa wasiogope waendelee kupaza sauti.

Professor Jay amesema kuwa kesi hiyo itaendelea kusikilizwa leo ambapo RCO na RPC wa Mbeya watasimama kutoa ushahidi wao.
SUGU kaniambia niwaambie ‘MSIOGOPE’ bali endeleeni kupaza Sauti!!Kesi yao inaendelea leo saa Tatu asubuhi hii katika mahakama kuu ya Mbeya, ambapo RCO na RPC wa Mbeya watasimama kutoa ushahidi wao LEO,” ameandika Proffesor Jay kwenye ukurasa wake wa Insta.
Sugu anakabiliwa na kesi ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais Magufuli. Ambayo wanadaiwa kuitoa Disemba 30 kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment