Viongozi wa upinzani wapokonywa hati za kusafiria na maafisa uhamiaji

Viongozi 14 wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA) wamepokonywa hati zao za kusafiria (Passport) na Idara ya Uhamiaji.

Viongozi hao ni pamoja na Gavana wa Kaunti ya Mombasa, Hassan Ali Joho na viongozi wengine ni Mfanyabiashara Jimmy Wanjigi, James Orengo, David Ndii na baadhi ya makada wa NASA.
Bado serikali haijatoa sababu ya kushikilia passport hizo lakini Vyombo vya Habari nchini humo vimehusisha tukio hilo na sababu za kisiasa.
Wakati hayo yakijiri jana Februari 7, 2018 wafuasi wa NASA waliandamana kushinikiza serikali kumrudisha nchini Kenya mwanaharakati, Miguna Miguna ambaye amefukuzwa nchini humo kwa kuhudhuria siku ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment