WCB haina tatizo na media yoyote, Ruge ndio mwenye tatizo na WCB – Sallam

Meneja wa label ya WCB, Sallam SK amefunguka kwa kuendelea kudai kwamba kampuni yao haina tatizo na chombo chochote cha habari isipokuwa Ruge Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds FM na Clouds TV ndio mwenye tatizo na label hiyo.


Mapema wiki hii meneja huyo alianza kwa kuandika ujumbe mtandaoni unaodai kuna mtu anataka kumshusha Diamond huku akidai hakuna mtu wa kumshusha katika utawala huu wa Rais John Pombe Magufuli.

Sallam ameendeleza mashambulizi hayo ambapo jana amemtaja mtu aliyedai kwamba ana njama za kumshusha Diamond.

“Kwa heshima ya Joe Kusaga kukuombea msamaha kwa leo Bw Ruge Mutahaba naamua kukusitiri, ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi nitayaanika maovu yako yote unayoyafanya kwenye Industry ya muziki. WCB haina tatizo na media yoyote na wala haina tatizo na Clouds Media Group ila huyu Ruge Mutahaba ndio mwenye tatizo #TumekataaKuwaKaa,” aliandika Sallam kupitia Instagram.

Meneja huyo anaonekana kutaka kuendeleza harakati hizo kwani toka aanze kutoa waraka huo amekuwa akiweka hushtag ambayo imekuwa ikitumika na Clouds Media, #TumekataaKuwaKaa.

Ruge bado hajazungumza chochote kuhusiana na tukio hili lakini Bongo5 tunafanya jitihada za kumtafuta ili kusikiliza kwa upande wake.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment