Abdul Nondo apewa dhamana Iringa

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Iringa kupitia kwa Hakimu wake John Mpitanjia imeweka wazi dhamana kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo.

Hakimu Mpitanjia ametoa masharti ya dhamana hiyo kwa Nondo ni kuwa na watu watakao mdhamini ambao ni wakazi wa Iringa, mmoja awe anafanya kazi serikalini, wawekebondi ya shilingi milioni tano na wawe na mali isiyohamishika.
Hata hivyo wakili wa Nondo, Jebra Kambole anashughulikia dhamana hiyo. Wakati huo huo kesi hiyo imeahirishwa mpaka April 4 ya mwaka huu.
Nondo anashtakiwa kwa makosa mawili ikiwemo kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni March 7 ya mwaka huu kuwa maisha yake yapo hatarini akiwa katika eneo la Ubungo na kuzisambaza kwenye mtandao wa Whatsapp.
Kosa la pili limetajwa kuwa ni kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga wakati alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini humo kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment