Dimaond Amuahidi Mama yake kufunga ndoa Mwaka huu

Msanii wa muziki Diamond Platnumz amemuahidi mama yake kufunga ndoa mwaka huu na kuachana na mambo ya ujana ambayo amedai yanamchukiza mama yake. Mwimbaji huyo alitoa taarifa hiyo jana wakati akimtakia heri mama yake katika siku ya wanawake duniani.

Alipost picha ya mama yake na kuweka caption hii
Happy Women's day Mama na wanawake wote Ulimwenguni... Nashkuru sana kwa kunizaa na kunilea...Wewe ni Mboni na Nguzo ya Maisha yangu mama...Licha ya shida na Mateso uliyoyapata kwenye kunizaa na kunilea, lakini hata sasa ambapo ulitakiwa walau Upumzike nimekuwa nikikukosea kwa kukuingiza hata kwenye Matatizo Yasiyokuhusu...Wanakutukana, wanakukebehi na kukutupia kila neno lililo baya, yote kwa sababu yangu mimi, lakini sikuzote umekuwa mwenye kunisamehe, kunipenda na Kunithamini.....Nakupenda sana Mama, Na nisameh kwa yote nilokukosea... Inshaalah, Mwenyez Mungu anibariki Mwaka huu Mwanao nifanikishe Ndoa yangu na kukupa Furaha ya Milele ambayo siku zote umekuwa Ukiitaka..... @mama_dangote

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment