Hamna chochote kati yangu na Nandy – Aslay

Msanii wa muziki Bongo, Aslay amefunguka kuhusu ukaribu wake na Nandy kwa sasa.

Muimbaji huyo wa ngoma ‘Natamba’ ameiambia FNL ya EATV kuwa kinachowaunganisha ni kazi tu hakuna mahusiano ya kimapenzi kama inavyokuwa ikiripotiwa.
“Nafikiri mashabiki zangu ambao wananifuatilia wanajua ni mtu ambaye nina mtoto, kuna mwanamke ambaye nimezaa naye. Nandy tupo kwenye kazi tu, tunafanya lakini hamna chochote kinachoendelea kati yangu na Nandy,” amesema.
Aslay na Nandy kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma ‘Subalkheri’ ikiwa ni ngoma yao ya pili kutoa pamoja baada ya Mahabuba.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment