Hata tukiwa Wananchi milioni 1 kama hatufanyi kazi vyuma vitaendelea kubana – Rais Magufuli

Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewajibu watu ambao wanaendelea kusema kauli za vyuma vimekaza.

Rais Magufuli ambaye leo (Jumatano) amezinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kiwango cha Standard Gauge kutokea Morogoro mpaka Makotopora, Dodoma, amesema hata tukiwa watu milioni moja katika nchi bado hali itakuwa kama hivyo endapo tutazembea kufanya kazi.
“Hata tukiwa Wananchi milioni moja tu , kama hatufanyi kazi vyuma vitaendelea kubana tu! Kubwa hapa ni kuchapa kazi tujiletee maendeleo,” amesema Rais Magufuli.
“Haya tunayoyafanya sasa hayajalishi mimi nipo kama rais. Nyerere alifanya akaondoka, Mwinyi, Mkapa na Kikwete wote wamefanya na wameondoka. Utafika wakati na mimi nitaondoka, lakini vizazi vijavyo watavikuta nilivyovifanya na kujivunia,” ameongeza.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment