Mimi Mars aeleza ukweli wa kutoka kimapenzi na Diamond

Msanii wa muziki Bongo, Mimi Mars amefunguka ukweli wa taarifa zilizodai alikuwa akitoka kimapenzi na Diamond Platnumz.

Mimi Mars amelazimika kuzungumzia hilo mara baada ya video iliyowahi kusambaa katika mitandao ikionyesha akicheza wimbo wa Diamond unaokwenda kwa jina la Eneka.
Muimbaji huyo kutoka label ya Mdee Music ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote ila alichofanya yeye ni kucheza wimbo wa msanii huyo pekee na alikuwa hajua kama ni wa Diamond kwa wakati huo.
“Haina ukweli kabisa, kwanza cha kushangaza ni kwamba wakati nilikuwa nacheza huo wimbo nilikuwa hata sijajua kama ni wa Diamond,” amesema Mimi Mars.
“Nilikuwa nimeenda kwa fundi kuchukua ile nguo ambayo nimeivaa, kwa hiyo akaweka muziki akasema ebu cheza kidogo, so I was just dance the song mpaka baadaye nipo kwenye gari ndio najua huo wimbo ni wa Diamond, it was too late na ile video ilienda, kwa hiyo kulikuwa hamna ishu yoyote,” amesisitiza.
Ameongeza kuwa anataka kusikika na kuonekana katika masikio na macho ya mashabiki lakini si kwa mtindo huo na ni kitu kilichomsumbua kidogo. Mimi Mars kwa sasa anatamba na ngoma mpya inayokwenda kwa jina la Papara.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment