Mjasiriamali Maria Tsarungi kumburuza mahakamani mhariri wa gazeti la Tanzanite


Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi amefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Mhariri wa Gazeti la Tanzanite na Mwanasheria Cyprian Musiba kwa kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliyofanyika tarehe 25 Februari, 2018.

Maria Sarungi
Barua hiyo iliyotolewa na Mwanasheria wa Maria Sarungi, Benedict Alex Ishabakaki imeeleza kuwa mteja wake alitajwa na gazeti la Tanzanite toleo Namba 50 lililotoka Februari 26, 2018 kuwa ni moja ya watu hatari kwenye usalama wa taifa.
Kwa upande mwingine, barua hiyo imeitaka Blog ya Dar24 kufuta habari hiyo na kuomba radhi hadharani kwa kitendo cha kuandika habari hiyo yenye lengo la kumfedhehesha mteja wao.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment