Wabunge wengine CHADEMA walala rumande

Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Susan Kiwanga wa Mlimba, na Peter Lijualikali (Kilombero) wamerudishwa rumande na mahakama ya Hakimu Mkazi Nkoa wa Morogoro ambapo wanasubiri hadi Marchi 7, 2019 itatoa uamuzi wa dhamana yao.

Kiwanga na Lijualikali wamefikishwa Mahakamani leo Jumatatu Machi 4, 2019 ambapo kesi yao ilianza kusikilizwa leo kupitia kwa Hakimu Elizabert Nyembele.
Akizungumza wakati kesi hiyo ikiendelea upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Hekima Mwasipu ulipinga zuio la dhamana lililotolewa na upande wa mashtaka ambapo wamedai zuio hilo halikufuata taratibu za kisheria.
Akijibu madai hayo wakili Mwasipu amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuonyesha kifungu maalumu walichokitumia katika kupinga dhamana ya washtakiwa.
Mpaka sasa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA), Freemani Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wako rumande kutokana na makosa ya kukiuka masharti ya dhamana
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment